"Mvua inaponyesha, tunalowa kama kuku. Maisha tunayoishi hapa ni mabaya sana. Chawa walioko kwenye nguo zetu wanatufanya tuugue kutokana na ukosefu wa usafi. Bado tumevaa nguo zile zile ambazo tulikuwa tumevaa tukiondoka nyumbani kwetu," amesema Neema Amosi anaeishi kambini Burundi baada ya kukimbia machafuko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Imeelezwa kuwa Neema ni miongoni mwa waathirika wa mapigano yanayofanyika DRC kati ya waasi waliojihami kwa silaha na Jeshi la serikali, na anaishi na Wakongo wengine katika kambi ya wakimbizi ya Cishemere eneo la Cibitoke, Nchini Burundi, karibu na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Neema anasema anaishi katika nyumba moja ndogo iliyojengwa na nyasi kwa sababu hakufanikiwa kupata hema katika kambi hiyo. Anaishi na watoto wake watano, na Jirani yake ambaye alimsaidia kukimbia nyumbani kwao eneo la Luvungi, nchini DRC.
Pia imeelezwa katika kambi ya Cishmere, takribani raia 8,500 wa DRC wanaishi hapo wakitarajia kuhamishwa na kupelekwa katika kambi zenye mazingira bora za Busuma eneo la Ruyigi.
Chanzo; Nipashe
Chawa Watesa Wakimbizi Congo
- Chanzo:
- Nipashe