Rais Donald Trump ameonya kuwa Marekani inaweza kufanya mashambulizi mengine ya anga nchini Nigeria ikiwa mauaji ya Wakristo yataendelea.
Katika mahojiano na gazeti la New York Times, lililochapishwa siku ya Alhamisi, Trump aliulizwa ikiwa mashambulizi ya hivi majuzi ya anga ya Marekani katika jimbo la Sokoto nchini Nigeria yakilenga wanamgambo wenye itikadi kali yalikuwa sehemu ya operesheni kubwa zaidi ya kijeshi.
Akijibu swali hilo, Trump alisema: “Ningependelea liwe shambulio la mara moja.” Hata hivyo, aliongeza kwa msisitizo: “Iwapo mauaji dhidi ya Wakristo yataendelea, basi yatakuwa mashambulizi ya mara kwa mara.”
Utawala wa Trump hapo awali umeikosoa vikali Serikali ya Nigeria kwa kile ilichokitaja kuwa kushindwa kuwalinda Wakristo dhidi ya mashambulizi ya wanamgambo wa jihadi.
Chanzo; Itv