Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema yeyote anayetaka kushindana na Urusi kijeshi "awe huru kujaribu", akisisitiza kuwa taifa hilo ambalo liliivamia kijeshi Ukraine litalinda maslahi ya watu wake na uwepo wa dola hilo.
“Ikiwa kuna mtu anataka kushindana nasi kijeshi basi anaweza kujaribu, Urusi imeendelea kulinda uwepo na uhalisia wake, tutajibu haraka.” - Putin
Ameonya kuwa mara kadhaa Urusi inapokabiliwa na kitisho majibu yake huwa makali.
Wachambuzi wa siasa za Ulaya wameitafsiri kauli hiyo kama onya kwa mataifa ya Magharibi yanayoiunga mkono Ukraine.
Chanzo; Dw