Utafiti mpya uliofanywa na Taasisi ya Kitaifa ya Utafiti wa Tiba Kenya (KEMRI) kwa ushirikiano na wanasayansi wa kimataifa umebaini kuwa mabadiliko ya tabianchi yamesababisha kubadilika kwa tabia za mbu aina ya Anopheles Funestus, wanaoeneza ugonjwa wa malaria.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mbu hawa sasa wameanza kung’ata mchana kinyume na desturi yao ya kung’ata usiku, na pia wanaonesha ukinzani mkubwa dhidi ya dawa zinazotumika kuwadhibiti.
Chanzo: Dw