Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Rais Amteua Marehemu Kimakosa Kwenye Kamati ya Uchaguzi

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, amemteua bila kukusudia Steward Sorobia Budia, aliyefariki dunia, kuwa mjumbe wa kamati itakayohusika na maandalizi ya uchaguzi wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa msemaji wa Ofisi ya Rais, makosa yalitokea katika mchakato wa uteuzi baada ya jina la Budia, mwanasiasa wa zamani wa upinzani, kujumuishwa miongoni mwa wajumbe waliotajwa katika amri ya rais.

Taarifa zinaeleza kuwa Budia alifariki dunia takribani miaka mitano iliyopita.

Aidha, familia ya marehemu imeripotiwa kudai fidia, ikieleza kuwa kwa mujibu wa tamaduni zao, hairuhusiwi kumtaja au kuamsha roho ya marehemu bila ridhaa au ushiriki wa familia.

 

 

Chanzo; Crown Media

Kuhusiana na mada hii: