Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Schwarzenegger Ayataka Mataifa Kuthamini Utunzaji Mazingira

Aliyekuwa Gavana wa California na mwigizaji mashuhuri wa filamu Arnold Schwarzenegger amesema mataifa duniani na taasisi za dini wanayo nafasi kubwa kuchochea ushawishi katika kutunza mazingira akitolea mfano wa Kanisa Katoliki lenye waumini bilioni 1.4 duniani kote.

Viongozi zaidi ya 1,000 wa dini, wataalamu wa hali ya hewa na viongozi wa kisiasa wanakutana mjini Castel Gandolfo, Italia katika mkutano wa “Raising Hope for Climate Justice” unaofanyika Castel Gandolfo kuanzia leo Jumatano Oktoba 1 hadi 3, 2025.

Schwarzenegger amezungumza kuhusu azma yake ya kuunganisha serikali na wanaharakati wa ngazi ya chini kwa ajili ya kuhimiza utunzaji mazingira.

Amesema Mungu amempa kipaji cha kuwasilisha ujumbe wa mazingira na anaamini atafanya kila niwezalo kuifanya dunia hii kuwa bora zaidi.

Schwarzenegger amesema mataifa yanayotekeleza kwa vitendo utunzaji mazingira ndio mashujaa wa kweli wa vitendo.

Pia, ametoa wito wa kupuuza waliokata tamaa wanaodai kuwa sheria za mazingira zinaathiri uchumi. Alieleza kuwa jimbo la California lina uchumi unaoendelea kwa kasi licha ya kuwa na sheria kali zaidi za mazingira.

 

Chanzo: Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: