Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Wanajeshi wa Marekani Watua Nigeria Kutoa Msaada

Nchi ya Nigeria inasema takriban wanajeshi mia moja wa Marekani wamewasili kusaidia kutoa mafunzo kwa wanajeshi wake.

Nigeria iliomba usaidizi wa mafunzo, kiufundi na ushirikiano wa kijasusi baada ya Rais Trump kuishutumu kwa kushindwa kuwalinda Wakristo dhidi ya mashambulizi kijihadi.

Msemaji wa ulinzi wa Nigeria amesema takriban wanajeshi 100 wa Marekani wamewasili nchini Nigeria huku Marekani ikiimarisha operesheni ya kuwalenga waasi wa Kiislamu.

Rais wa Marekani Donald Trump ameishutumu Nigeria kwa kushindwa kuwalinda Wakristo dhidi ya wanamgambo wenye itikadi kali za Kiislamu kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Hata hivyo, Nigeria imekanusha kubagua dini yoyote ikisema vikosi vyake vya usalama vinalenga makundi yenye silaha ambayo yanashambulia pande zote mbili Wakristo na Waislamu.

 

 

Chanzo; Itv

Kuhusiana na mada hii: