Siku mbili baada ya Marekani kumkamata Rais Nicolas Maduro wa Venezuela kutoka Ikulu ya nchi hiyo mjini Caracas, maelfu ya wafuasi wake wameingia mitaani kulaani tukio hilo.
Tukio la kukamatwa Maduro na mkewe na kisha kupelekwa Marekani kujibu madai ya kufadhili mtandao wa kuuza dawa za kulevya, limesababisha mgawanyiko mkubwa nchini Venezuela.
Wale walioshuhudia ukandamizaji wa utawala wa Maduro wamefurahia kilichotokea huku wafuasi wa kiongozi huyo wakilaani vikali kukamatwa kwake.
Chanzo; Dw