Watu sita wamefariki dunia baada ya helikopta kuanguka na kulipuka kwa moto katika eneo la Chepkiep, Kaunti Ndogo ya Mosop, Kaunti ya Nandi, leo Jumamosi, Februari 28, 2026.
Kulingana na mkuu wa polisi katika Kaunti hiyo Samuel Mukuusi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na utambuzi wa waliofariki unaendelea.
Kwa mujibu wa taarifa za awali, helikopta hiyo ilikuwa na abiria sita wakati ilipoanguka.
Kwa sasa, taarifa kutoka Nandi zinaeleza kuwa nambari ya usajili wa helikopta hiyo ni 5Y-DSB, inayomilikiwa na kampuni yenye makao yake katika Uwanja wa Ndege wa Wilson, Nairobi.
Kwa mujibu wa taarifa za mtandao wa kufuatilia safari za ndege wa Flightradar24, chombo hicho ni aina ya Airbus Helicopters H125 na kiliwahi kutumiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani nchini humo mnamo Septemba 15, 2025.
Chanzo; Eatv