Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

China Yazindua Daraja Refu Zaidi Duniani

China imezindua rasmi Daraja la Huajiang Grand Canyon linalotajwa kuingia kwenye rekodi ya Dunia ya Daraja lililo refu zaidi kwenda juu likiwa na mita 625 kutoka usawa wa chini ya korongo ambapo kukamilika kwake kumetajwa kupunguza muda wa kuvuka korongo kutoka dakika 120 hadi dakika mbili pekee.

Tukio la uzinduzi limefanyika Septemba 28 ambapo Vyombo vya habari vya Serikali hiyo vilirusha matangazo ya moja kwa moja na kuhudhuriwa na mamia ya Watu wakiwemo Wahandisi wa mradi, Viongozi wa Serikali na Wakazi wa eneo hilo.

Daraja la Huajiang lina urefu wa jumla ya mita 2,900 huku likiwa na kipande kikuu cha mita 1,420 ambapo sasa linashikilia rekodi mbili muhimu ikiwemo ya daraja refu zaidi duniani kutoka usawa wa chini ya ardhi ambapo kabla ya kufunguliwa, daraja hilo lilifanyiwa majaribio makali ya uthabiti ambapo Wahandisi walitumia Malori 96 yaliyosambazwa sehemu mbalimbali za daraja ili kupima uzito wa magari makubwa huku zaidi ya sensa 400 zikitumika kupima viwango vya daraja hilo.

Zaidi ya kuwa njia ya mawasiliano, daraja hilo limebuniwa pia kama kivutio cha utalii, linajumuisha lifti ya utalii yenye mita 207, sky cafes, na Vituo vya kutazama mandhari vinavyotoa muonekano wa kuvutia wa korongo hilo.

 

Chanzo: Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: