Mkuu wa Jeshi la Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, amesema jeshi la Uganda halipigi wanawake kama kiongozi wa upinzani, Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine anavyodai.
Jenerali Kainerugaba ambaye pia ni mtoto wa Rais Yoweri Museveni, amebainisha hayo akijibu tuhuma za wanajeshi wake kuvamia nyumbani kwa Bobi Wine na kuwatesa watu na kumpiga mke wake.
“Jeshi letu haliwapigi wanawake,” ameandika Kainerugaba.
Bobi Wine alidai kwamba askari walivamia makazi yake usiku katika kitongoji cha Magere jijini Kampala, waliwadhalilisha baadhi ya wafanyakazi na kumkaba mke wake.
Kiongozi huyo amesema hakuwepo nyumbani wakati wa tukio hilo kwani tangu uchaguzi wa urais ulioibua utata nchini humo ameendelea kuishi mafichoni ili kuepuka kushikiliwa.
Chanzo; Mwananchi