Mamlaka za Gaza zimesema watu wasiopungua 85 wameuawa katika Ukanda wa Gaza katika kipindi cha saa 24 zilizopita. Aidha Israel imeendeleza operesheni yake ya kijeshi katika jiji la Gaza huku maelfu ya Wapalestina wakiendelea kuondoka katika jiji hilo.
Mashambulizi hayo yamepelekea kukatika kwa umeme na mawasiliano ya simu na intaneti. Hayo yakiarifiwa, Marekani kwa mara nyingine tena imetumia kura yake ya turufu hapo jana Alhamisi kuzuia kupitishwa kwa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililotaka kusitishwa kwa mapigano huko Gaza, kuwezesha ufikiaji wa misaada ya kibinadamu na kuachiliwa kwa mateka.
Chanzo; Dw