Muswada wa sheria yenye utata utakaoanzisha adhabu ya kuwanyonga magaidi umevuka hatua ya kwanza ndani ya Bunge la Israel, Knesset.
Muswada huo unaoungwa mkono na serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, ulipitishwa baada ya kusomwa mara ya kwanza bungeni leo Jumatatu. Ili kuwa sheria kamili, muswada huo itafaa uvuke hatua nyingine mbili bungeni.
Ukishakuwa sheria, utaruhusu kutolewa adhabu ya kifo kwa watu watakaotiwa hatiani kuwaua Waisraeli kwa sababu za “ubaguzi wa rangi na uhalifu mwingine wenye lengo la kuidhuru Israel au uhalali wa Wayahudi kuwa na taifa lao”.
Wakosoaji wake wanasema muswada huo unalenga kuwaadhibu Waarabu wanaowaua Wayahudi na siyo Wayahudi wenye misimamo mikali wanaowashambulia na hata kuwaua kila wakati Wapalestina.
Chanzo; Dw