Rais wa Kenya William Ruto amezua gumzo mitandaoni baada ya kuonekana akitembea kwa miguu wakati wa ziara yake ya hivi karibuni nchini Marekani.
Picha za mtandaoni zilimuonyesha kiongozi huyo akitembea barabarani pamoja na ujumbe wake, huku wengi wakitoa maoni tofauti kuhusu tukio hilo.
Wengine wametafsiri tukio hilo kama ishara ya unyenyekevu na uongozi wa karibu na wananchi, wakisema ni mfano wa kiongozi anayejiepusha na fahari isiyo ya lazima. Hata hivyo, baadhi waliona ni tofauti kubwa na misafara mikubwa ya magari anayotumia akiwa nyumbani.
Mjadala umeibuka kuhusu tofauti ya mienendo ya viongozi wa Afrika wanapokuwa nyumbani na wanapofanya ziara nje ya bara, hasa Ulaya.
Chanzo: Dw