Rais wa Venezuela, Nicolàs Maduro yupo jijini New York, Marekani anakoshikiliwa baada ya kutekwa na Vikosi vya Marekani ambapo leo Jumatatu, anatarajiwa kupandishwa mahakamani na kusomewa mashtaka yanayomkabili.
Utawala wa Maduro nchini Venezuela, ulitawaliwa na changamoto nyingi kati yake na wapinzani, wakosoaji, wanaharakati na raia wa kawaida.
Miongoni mwa mambo ambayo Maduro alikuwa akilalamikiwa sana, ni pamoja na kudorora kwa kiasi kikubwa kwa uchumi licha ya nchi hiyo kuwa na utajiri wa rasilimali na ukandamizwaji wa demokrasia, kusakamwa kwa wapinzani na kufanyika kwa chaguzi zisizokuwa za haki.
Mfumuko wa bei, upungufu mkubwa wa bidhaa muhimu kama chakula, dawa na mahitaji mengine ya kibinadamu vikachangia wananchi maskini wa Venezuela kuendelea kula msoto mkali kila kukicha.
Chanzo; Global Publishers