Bunge la Ulaya limepitisha pingamizi dhidi ya mpango wa Tume ya Ulaya wa kuelekeza msaada wa kifedha kwenda Tanzania kupitia mfuko wa NDICI-Global Europe hatua inayotajwa kuchochewa na matukio ya kisiasa yaliyotokea nchini kuanzia Oktoba 29 mwaka huu.
Hatua hiyo ni matokeo ya kura zilizopigwa na Kamati ya Mambo ya Nje ya bunge hilo kuhusu kuzuia utekelezaji wa mpango huo ambapo kura 53 zilikubali pingamizi hilo huku 2 zikipinga wakati kura moja ikiharibika.
Tume ya Ulaya ilipanga kutuma zaidi ya Euro Milioni 150 sawa na zaidi ya Sh bilioni 400 kwenda Tanzania mwaka 2026, kwa ajili ya miradi ya maendeleo ambapo utekelezaji wa msaada huo haukuzingatia hali halisi ya haki za binadamu na utawala wa sheria nchini Tanzania.
Chanzo; Nipashe