Mnamo mwaka 1986, Rais Yoweri Museveni alisema bara la Afrika linashindwa kujikwamua kutoka kwenye umasikini kutokana na viongozi kung’ang’ania madarakani.
Hivi sasa Museveni amedumu katika wadhifa wa Rais kwa takribani miaka 40 na anawania muhula wake wa saba.
Utawala wake umekuwa ukishutumiwa kwa rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na ubadhirifu wa mali za umma.
Katika uchaguzi huu, Museveni anasema ni muhimu kwa Waganda kumchagua ili kulinda mafanikio yaliyopatikana, huku mpinzani wake mkuu Bobi Wine akiwahimiza wananchi kuunga mkono mabadiliko ya kimfumo.
Chanzo; Dw