Tirana, Albania imerekodi rekodi ya dunia kwa kuwa nchi ya kwanza kuteua waziri aliyeundwa kwa akili bandia (AI), siyo waziri wa teknolojia ya AI, bali waziri halisi wa kidijitali, aliyeundwa kwa misimbo na kuendeshwa na mfumo wa kisasa wa akili bandia.
Jina lake ni Dieella, linalomaanisha 'mwanga wa juu' kwa Kialbania ndilo jina la roboti, atasimamia shughuli zote za manunuzi ya umma, kama alivyoeleza Waziri Mkuu Edi Rama.
Aliteuliwa rasmi Alhamisi ya Septemba 11, 2025, ambapo Rama alimtambulisha kama"mwanachama wa baraza la mawaziri asiye na uwepo wa kimwili," ambaye atahakikisha kuwa zabuni za umma zitakuwa huru kwa asilimia 100 dhidi ya ufisadi.
Chanzo: Mwananchi