Padri wa Kanisa Katoliki katika Kaunti ya Machakos aliondoka ghafla kwenye tukio la mazishi baada ya kuripotiwa kutofautiana na waombolezaji pamoja na familia ya marehemu kuhusu utaratibu wa ibada ya mazishi.
Kwa mujibu wa mashuhuda, mvutano uliibuka wakati wa maandalizi ya ibada, hali iliyosababisha padri huyo kuacha kuendelea na huduma na kuondoka eneo la mazishi.
Tukio hilo liliacha sintofahamu miongoni mwa waombolezaji na familia huku mazishi yakiendelea kwa mpangilio mwingine.
Mpaka sasa hakuna tamko rasmi kutoka kwa mamlaka za kanisa kueleza kilichosababisha mvutano huo huku wadau wakitoa wito wa mazungumzo na utulivu ili kuepusha matukio kama hayo siku zijazo.
Chanzo; Bongo 5