NASA imeripoti kugundua maumbo yanayofanana na moyo katika maeneo mbalimbali ya mfumo wa jua, kuanzia sayari ya Mars hadi Pluto.

Kwa kutumia vyombo vya utafiti wa anga kama New Horizons, Mars Reconnaissance Orbiter, na Curiosity Rover, wanasayansi wameona maumbo hayo kwenye mabonde, mashimo (craters), maeneo yenye mwanga mkali, pamoja na ardhi za milimani.
Ugunduzi huu unaonyesha jinsi maumbile ya ulimwengu yanavyoweza kuunda maumbo yanayofanana na alama tunazozifahamu, jambo linaloendelea kuwavutia wanasayansi na wapenda masuala ya anga duniani kote.
Chanzo; Global Publishers