Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Palestina Yanukia Ummoja wa Mataifa

Dalili za uhuru wa Palestina zazidi kuonekana, kufuatia uungwaji mkono wa karibu mataifa 150, ikiwemo nchi nne zenye kura ya turufu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambazo sasa zimetambua rasmi taifa hilo.

Chini ya Mkataba wa Montevideo wa mwaka 1933, kuna vigezo ili Palestina itambuliwe kuwa taifa huru chini ya sheria ya kimataifa, inahita kukidhi vigezo kdhaa.

Licha ya kutosaini Mkataba wa Montevideo wa mwaka 1933, Uingereza imetangaza rasmi kulitambua taifa la Palestina, na kuadhimisha hatua hiyo kwa kuzindua ubalozi wake jijini London, ambapo bendera ya Palestina ilipandishwa wiki hii kwa mara ya kwanza.

Taifa la Palestina limetambuliwa rasmi na mataifa 151 kati ya 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na zaidi ya nchi 12 kutoka barani Ulaya, zikiwemo Hispania, Ireland na Norway.

Hata hivyo, ili Palestina iwe mwanachama kamili wa Umoja wa Mataifa inatakiwa ithibitishwe kwa angalau kura tisa za wajumbe wa Baraza la Usalama na si kura ya veto.

Baraza la Usalama lina wajumbe 15, huku watano wakiwa wa kudumu ambao ni Uingereza, Marekani, Ufaransa, Russia na China.

Kwa sasa, wajumbe 10 wa muda wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kipindi cha miaka miwili ni Algeria, Denmark, Ugiriki, Guyana, Pakistan, Panama, Jamhuri ya Korea, Sierra Leone, Slovenia na Somalia.

 

Chanzo: Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: