Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Kijana Miaka 13 Aogelea Kilometa 4 Kumfata Mama Yake Baharini

Mvulana wa miaka 13 amesifiwa baada ya kuogelea katika maji yenye mawimbi na mwanga hafifu ili kumwokoa Mama yake na ndugu zake wawili waliokuwa wamebebwa na maji baharini karibu na pwani ya Australia.

Polisi wa Australia wanasema familia hiyo ilikuwa ikiendesha ubao wa kuteleza kwenye maji huko Geographe Bay, karibu na Quindalup Magharibi mwa Australia, siku ya Ijumaa wakati upepo mkali ulipowapeleka mbali.

Kijana huyo alianza kupiga makasi ili kurudi ufukweni ili kutoa taarifa lakini mtumbwi wake aina ya kayaki uliingia maji kwa hivyo aliogelea kilomita nne zilizobaki hadi ufukweni.

"Ushujaa, nguvu na ujasiri ulioonyeshwa na familia hii ulikuwa wa ajabu, hasa kijana aliyeogelea kilomita nne ili kutoa taarifa," kimesema Kikundi cha Uokoaji Majini cha Naturaliste.

Kamanda wa kikundi hicho Paul Bresland amesema, aliogelea kwa saa mbili za kwanza akiwa amevaa koti la kuokoa maisha.

"Kijana huyo alifikiri hatafanikiwa akiwa amevaa koti la kuokoa maisha, kwa hivyo aliliacha, na akaogelea saa mbili zilizofuata bila koti la kuokoa maisha,” amesema.

Polisi wa Australia Magharibi walisema katika taarifa, wamesema mvulana huyo aliweza kutoa taarifa Ijumaa jioni, na kusababisha msako kutoka kwa mashirika mbalimbali.

Mama huyo mwenye umri wa miaka 47, mwanawe mwingine wa kiume, 12, na binti yake mwenye umri wa miaka nane, walipatikana na helikopta ya uokoaji wakiwa wameshikilia ubao wa kuogelea kama kilomita 14 kutoka ufukweni.

"Meli ya uokoaji ya kujitolea ilielekezwa mahali walipo na wote watatu waliokolewa na kurudishwa ufukweni," kikosi hicho kimesema.

 

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: