Kwa mujibu wa tafti mpya zinaonyesha sekta ya pombe duniani imepoteza takriban $830 bilioni katika miaka minne iliyopita, huku kizazi cha Gen Z kikitajwa kuongoza mabadiliko ya mtazamo kuhusu unywaji.
Wengi wa kizazi hicho wameamua kunywa kwa uangalifu zaidi, kupunguza au kuacha kabisa, wakipa kipaumbele afya ya akili, ustawi, na maisha bila pombe. Hali hiyo imesababisha kushuka kwa mauzo ya bia, divai na pombe kali, na kuongezeka kwa umaarufu wa mocktails, vinywaji visivyo na kilevi na vyenye kiwango kidogo cha pombe.
Kampuni kubwa za pombe sasa zimeanza kuwekeza kwenye bidhaa zisizo na kilevi, wakikiri kuwa huu si mtindo wa muda mfupi bali ni mabadiliko ya kijamii yanayoathiri tasnia nzima.
Chanzo; Nipashe