Kipande cha video kinachoonyesha Rais wa Marekani Donald Trump akionekana akionesha alama ya kidole cha kati, kitendo kinachotafsiriwa kama matusi, kwa mfanyakazi wa kiwanda cha magari cha Ford.
Kwa mujibu wa video hiyo, mfanyakazi huyo alimpigia Trump kelele akimtuhumu kuwa “mlinzi wa wabakaji wa watoto,” kauli iliyosababisha tukio hilo.
Baada ya kusambaa kwa video hiyo mitandaoni, mjadala mkubwa umeibuka kuhusu mwenendo wa rais.

Ikulu ya Marekani (White House) imetetea kitendo cha Trump, ikisema hatua hiyo ilikuwa “sahihi kulingana na mazingira,” kauli ambayo imezidi kuchochea mijadala kuhusu mipaka ya maadili na namna viongozi wakuu wanavyopaswa kujibu ukosoaji kutoka kwa raia.
Chanzo; Cnn