Video ya abiria aliyekuwa ndani ya ndege aina ya ERJ145 wakati ikipata ajali ilipotua dharura katika uwanja wa Kolwezi, imezua mjadala mkubwa.
mpiga picha licha ya kutetemeka kwa kamera mara kadhaa, aliendelea kuielekeza kwenye tukio kwa ustadi wa kushangaza, ukizingatia mazingira hatarishi aliyokuwa ndani yake.
Abiria ameonyesha namna Watu walivyoshuka kwenye Ndege hiyo na namna inavyowaka moto baada ya kutua kwenye eneo ambalo sio barabara yake.
Ndege hiyo ilikuwa imekodishwa kuisafirisha ujumbe wa Wizara ya Madini, akiwamo Waziri wa Madini wa DR Congo, aliyekuwa safarini kuelekea Kolwezi kufuatilia ajali ya mgodi wa Kalando, ambapo tarehe 15 Novemba 2025, zaidi ya wafanyakazi 40 walipoteza maisha kufuatia kuporomoka kwa daraja kutokana na mvua kubwa.
Uwanja wa Ndege wa Kolwezi una mbio 11/29 yenye urefu wa mita 2,410 (sawa na futi 7,900) na hutumika zaidi na shughuli za mgodi wa shaba. Hata hivyo, eneo la kuanzia kutua katika mkondo wa 29 lilikuwa limesogezwa mbele kwa takribani mita 1,000 kutokana na kazi za ukarabati zinazoendelea, jambo linalotajwa kuwa chanzo kikuu cha tukio hilo.
Chanzo; Bongo 5