Afisa mmoja wa Iran amesema jana kwamba nchi hiyo italichukulia shambulizi lolote kwenye ardhi yake kuwa vita kamili dhidi ya jamhuri hiyo ya kiislamu.
Ametoa onyo hilo katika wakati msafara mkubwa unaojumuisha manuari ya kijeshi na meli za kivita za Marekani unaelekea eneo la Mashariki ya Kati.
Afisa huyo aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina, amesema wanatumai kwamba matayarisho hayo ya kijeshi hayakusudiwi kutumika kuishambulia Iran na kutahadharisha kuwa jeshi la nchi hiyo liko tayari kwa hali yoyote ile na litajibu kwa mapigo makali mashambulizi yoyote ya kigeni.
Chanzo; Dw