Ndege iliyombeba Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, kuelekea Florida, Marekani, kwa mkutano na Rais wa Marekani Donald Trump, imepita katika anga za Ugiriki, Italia na Ufaransa nchi wanachama wa Mkataba wa Roma unaotambua Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).
Kwa mujibu wa takwimu za FlightRadar, ndege hiyo iliingia Bahari ya Atlantiki baada ya kupita anga za mataifa hayo, licha ya kuwepo kwa hati ya kukamatwa dhidi ya Netanyahu iliyotolewa na ICC.
Safari hiyo ilifuata njia tofauti na ile aliyotumia Netanyahu mwezi Septemba mwaka huu alipokwenda New York kuhudhuria Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ambapo alitumia anga za Ugiriki na Italia pekee bila kuingia anga ya Ufaransa.
Hatua hiyo imeibua maswali mapya kuhusu utekelezaji wa wajibu wa nchi wanachama wa ICC na msimamo wao wa kisiasa katika kesi zinazohusu uhalifu wa kivita.
Chanzo; Cnn