Waziri wa usalama wa Venezuela, Diosdado Cabello, alisema usiku wa Jumatano kwamba watu 100 wamefariki katika shambulio la Marekani lililoondoa Rais Nicolás Maduro madarakani siku ya Jumamosi.
Hapo awali, mamlaka ya Venezuela hayakuwa yametoa idadi rasmi ya waliouawa, ingawa jeshi lilichapisha orodha ya majina 23 ya wanajeshi wake waliopoteza maisha.
Maafisa wa Venezuela wamesema kuwa sehemu kubwa ya kikosi cha ulinzi wa Rais Maduro kiliuawa huku Cuba ikithibitisha kuwa wanajeshi wake pamoja na maofisa wa ujasusi waliokuwa nchini Venezuela pia walifariki.
Cabello alisema kuwa mke wa Maduro, Cilia Flores, ambaye alikamatwa pamoja naye, alipata jeraha la kichwa wakati wa shambulio hilo, huku Maduro mwenyewe akipata jeraha mguuni, haya ni kwa mujibu wa Reuters.
Venezuela, ambayo Cabello aliisifu kama “jasiri” katika kipindi chake cha kila wiki kwenye runinga ya taifa, ilitangaza Jumanne wiki ya maombolezo kwa heshima ya wanajeshi waliouawa katika shambulio hilo.
Chanzo; Itv