Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Ahukumiwa Kifo kwa Kumuua Mwajiri Wake

Raia wa Uganda Vicky Ajok aliyekuwa akifanya kazi za ndani huko nchini Syria amehukumiwa kifo baada ya kukutwa na hatia ya kumuua aliyekuwa muajiri wake raia wa Syria.

Wakati hukumu hiyo ikitarajiwa kutekelezwa Februari 28, mwaka huu, Shirika la Migrant Workers Voice Uganda limewahimiza maofisa jijini Kampala kuzungumza na wenzao wa Syria ili kusimamisha utekelezaji wa hukumu hiyo dhidi ya Vicky.

Imeelezwa kuwa Vicky alihukumiwa kwa kumuua mwajiri wake mwenye umri wa miaka 87, Huda Shaarawi, ambaye ni mwigizaji maarufu wa tamthilia za televisheni nchini Syria.

Tukio hilo lilitokea mwezi uliopita katika mji mkuu wa Syria, Damascus.

 

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: