Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Maandamano ya Gen Z Yalitikisa Bara la Afrika

Afrika imekumbwa na shinikizo kubwa la maandamano ya vijana maarufuiru Gen Z,maandamano hayo yamekuwa yakibeba ujumbe wa vijana kupinga mifumo ya kiutawala,hali ya uchumi,haki za binadamu na matumizi ya rasilimali.

Kuibuka kwa maandamano ya vijana  katika baadhi ya mataifa barani Afrika kunatajwa kusukumwa zaidi na ukuaji wa teknolojia hususani mitandao ya kijamii ambayo imerahisisha uratibu na muunganiko wa vijana kutoka maeneo mbali mbali kujadili mustakabali wao na hata kutathmini utendaji wa serikali zao.

Makundi ya vijana kwa kutumia mitandao ya kijamii,yamekuwa yakijadili namna rasilimali za ndani ya mataifa yao zinavyotumika huku wengi wakilalamika kuishi kwenye umasikini katika utajiri mkubwa.

Afrika ina karibu 30% ya hifadhi ya madini duniani, ikiwa ni pamoja na cobalt, lithiamu na nikeli ambapo kwa mujibu wa Shirika la Nishati la Kimataifa linasema mahitaji ya lithiamu yanatarajia kukua mara tano ifikapo 2040 huku yale ya grafiti na nikeli yakitarajia kuongezeka kuongezeka maradufu nayo mahitaji ya cobalt  yakitarajiwa kuongezeka kwa asilimia 50% hadi 60% ifikapo 2040.

Wataalamu wa uchumi wanasema ili Afrika iweze kunufaika na mahitaji ya madini yake duniani haina budi kushughulikia suala la uhaba wa umeme,upungufu wa ujuzi,vikwazo vingi kwenye biashara pamoja na uwezo mdogo wa viwanda vya ndani

"Afrika inahitaji kujenga minyororo ya thamani ya ndani ambayo inaunganisha uchimbaji madini, uchenjuaji na na uvumbuzi, na hii inakwenda sambamba na mabadiliko ya uchumi unaojali mazingira " anasema Hany Besada,mwandamizi katika taasisi ya Firoz Lalji ya Afrika ambaye pia ni Mchumi na Profesa msaidizi wa Chuo Kikuu cha Wits.

Zimbabwe ni mzalishaji mkuu wa lithiamu barani Afrika, ambapo kwa siku za hivi karibuni imekuwa ikizishawishi kampuni za uchimbaji madini kuchakata madini hayo ili kusaidia kuujenga uchumi wa taifa hilo, hata hivyo wachumi wanasema bila kujenga mnyororo wa uchumi Afrika haitanufaika na utajiri wake kama anavyosema Besada

Afrika ilizindua eneo Huru la Biashara  (AfCFTA), yenye lengo la kuunganisha watu wote wapatao bilioni 1.4 kutoka  mataifa zaidi ya 50 na  kuwa na soko moja kwa ajili ya bidhaa za bidhaa na malighafi za ndani. Katika miaka ya hivi karibuni,ukanda wa Afrika ya magharibi umekumbwa na wimbi la tawala za kijeshi pamoja na kuibuka kwa mkakati maarufu uitwao utaifa wa rasilimali ambapo umekuwa ukiweka shinikizo kwa mataifa ya kigeni kuongeza thamani ya madini kutoka Afrika.

Vuguvugu la Kundi la vijana maarufu Gen Z  limekuwa likisambaa kwa kasi barani Afrika huku wakiweka shinikizo kwa serikali zao kutaka waone nao wananufaika na utajiri wa ndani ya mataifa yao huku wakiwanyooshea vidole vijana wasomi kutoka nje kuwa ni wanufaika wa utajiri uliomo ndani ya mataifa yao.

 

Chanzo; Dw

Kuhusiana na mada hii: