Rais wa Marekani, Donald Trump ameonya mamlaka ya Iran dhidi ya kuwaua wanaoandamana kwa njia ya amani, akisema taifa lake litaingilia kati.
Katika chapisho kwenye mitandao ya kijamii Trump aliandika: "Tuko tayari kwenda huko." Hakutoa maelezo zaidi.
Ofisa Mwandamizi wa Iran, Ali Larijani alijibu maoni ya Trump akionya kwamba kuingilia kati kwa Marekani katika masuala ya ndani ya Iran itakuwa sawa na kuyumbisha uthabiti wa eneo lote la Mashariki ya Kati.
Takriban watu sita wameripotiwa kuuawa nchini Iran siku ya Alhamisi baada ya karibu wiki moja ya maandamano makubwa yaliyosababishwa na hali mbaya ya kiuchumi.
Marekani ilishambulia vituo vya nyuklia vya Iran mwezi Juni, ikijiunga na kampeni ya anga ya Israeli iliyolenga mpango wa nyuklia wa Tehran na uongozi wa kijeshi.
Chanzo; Nipashe