Mahakama moja ya mji wa Istanbul, Uturuki, imetoa waranti wa kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na maafisa wengine 36 wa serikali yake kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya ubinadamu na mauaji ya halaiki kuhusiana na mzozo katika ukanda wa Gaza. Haya yameripotiwa na shirika la habari la serikali Anadolu.
Ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa Istanbul ilihalalisha hati hizo na kusema kwamba maafisa wa serikali ya Israeli wanapaswa kuwajibishwa kwa vitendo vya uhalifu dhidi ya ubinadamu na mauaji ya halaiki yaliyofanywa Gaza, pamoja na vitendo vilivyofanywa dhidi ya msafara wa kupeleka misaada katika Ukanda wa Gaza.
Mara kwa mara, Israel imeshutumiwa kwa uhalifu wa kivita na, katika baadhi ya matukio, mauaji ya halaiki juu ya matendo yake katika Ukanda wa Gaza, shutuma ambazo hata hivyo imekuwa ikizikanusha.
Chanzo; Dw