Ryan Routh amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kujaribu kumuua Rais Donald Trump kwenye uwanja wa gofu wa Florida mnamo Septemba 2024.
Routh, mwenye umri wa miaka 59, alipatikana na hatia mwaka jana ya kujaribu kumuua Trump, ambaye wakati huo alikuwa mgombea urais, katika Klabu ya Gofu ya Kimataifa ya Trump huko West Palm Beach.
Afisa wa Jeshi la Marekani katika eneo hilo aliona mtutu wa bunduki ukichomoza kutoka kwenye kichaka na kumpiga risasi Routh, ambaye alitoroka eneo la tukio na kukamatwa eneo la karibu.
Katika hati ya hukumu, Jaji Aileen Cannon alisema uhalifu wa Routh “bila shaka unastahili kifungo cha maisha”.
“Alichukua hatua kwa miezi kadhaa kumuua mgombea mkuu wa Urais, alionyesha nia ya kumuua mtu yeyote aliyemzuia, na tangu wakati huo hajaonyesha majuto wala kuhuzunishwa kwa waathiriwa wake,” aliandika.
Chanzo; Itv