Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mtoto wa Gadaffi Aripotiwa Kuuawa Libya

Ripoti za kushtua kutoka nchini Libya zinaeleza kuwa Saif al-Islam Gaddafi, mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gaddafi, ameuawa katika mji wa Zintan.

Kwa mujibu wa mwanasheria wake, Saif al-Islam alishambuliwa na kuuawa nyumbani kwake na watu wasiojulikana, katika tukio ambalo limezua taharuki kubwa nchini humo na kwenye anga za kimataifa.

​ Shambulio hilo lilitokea chini ya mazingira ya kutatanisha ambapo kamera za usalama katika makazi yake zilikuwa zimezimwa kabla ya wavamizi kutekeleza mauaji hayo.

Saif al-Islam, ambaye alikuwa akitazamwa kama mrithi wa kisiasa wa baba yake, amekuwa akiishi Zintan tangu kukamatwa kwake mwaka 2011, huku kifo chake kikihitimisha miongo kadhaa ya mvutano wa kisheria na kisiasa uliokuwa ukimkabili.

​Mpaka sasa, mamlaka nchini Libya bado hazijatoa tamko rasmi kuhusu wahusika wa shambulio hilo, huku hali ya usalama katika mji wa Zintan ikiripotiwa kuimarishwa zaidi.

Tukio hili linakuja wakati nchi hiyo ikiendelea kupambana na hali ya sintofahamu ya kisiasa na harakati za kuunganisha taifa hilo lililogawanyika.

 

Chanzo; Cnn

Kuhusiana na mada hii: