Marekani imetangaza kwamba itaanza kupunguza programu za msaada wa afya nchini Zimbabwe baada ya Zimbabwe kujiondoa kwenye mazungumzo kuhusu makubaliano ya afya ya pande mbili yenye thamani ya dola milioni 367.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyo tolewana Ubalozi wa Marekani ,ufadhili huo ungeunga mkono huduma muhimu za afya kama matibabu ya VVU/UKIMWI, kifua kikuu (TB), malaria, na huduma za afya ya uzazi na mama wajawazito.
Hatua hii inaashiria mabadiliko makubwa katika ushirikiano wa afya kati ya Marekani na Zimbabwe, na imezua mjadala mpana kuhusu masharti ya ufadhili, vipaumbele vya kitaifa, na mustakabali wa ushirikiano wa muda mrefu katika sekta ya afya.
Chanzo; Bongo 5