"Tulifanya uamuzi wa kufanya upasuaji kwa sababu tuliamini kwamba uume bado unaweza kuunganishwa tena, kulingana na muda uliopita tangu kukatwa,"
Madaktari katika hospitali ya Alert huko Addis Ababa wamefanikiwa kurudisha uume uliokatwa wa kijana mmoja baada ya upasuaji wa saa saba.
Madaktari wanasema mgonjwa, anapata nafuu na wanatarajia aanze kukojoa kawaida ndani ya wiki tatu, lakini kufanya mapenzi inaweza kuchukua takriban miezi mitatu.
Chanzo; Bbc