Wakulima nchini Ufaransa wameandamana kwa njia ya kushangaza kwa kumwaga takribani tani 30 za viazi nje ya jengo la Bunge la Taifa, wakipinga mkataba wa biashara huria unaopendekezwa kati ya Umoja wa Ulaya (EU) na MERCOSUR.
Waandamanaji wanasema makubaliano hayo yanahatarisha wakulima wa Ulaya kwa kufungua soko kwa bidhaa za kilimo kutoka Amerika Kusini, ambazo wanadai hazifuati viwango sawa vya uzalishaji.
Chanzo; Cnn