Daraja moja limeporomoka katika mgodi wa cobalt ulioko kusini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na kusababisha vifo vya wachimbaji 32 wa kujitegemea.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya afisa wa serikali ya mkoa.
Kulingana na afisa huyo, mkasa huo ulitokea Jumamosi katika eneo lililokuwa na mafuriko kwenye mgodi ulioko mkoa wa Lualaba.
Waziri wa mambo ya ndani wa mkoa huo, Roy Kaumba Mayonde, amesema miili 32 imepatikana na juhudi za uokoaji bado zinaendelea kutafuta wengine.
Inakadiriwa kuwa zaidi ya watu 200,000 hufanya kazi katika migodi mikubwa ya cobalt 'isiyo halali' katika taifa hilo la Afrika ya Kati.
Chanzo; Dw