Mwanaume mwenye silaha ameuawa kwa kupigwa risasi baada ya kukaribia eneo la makazi ya Rais wa Marekani Donald Trump huko Florida, imethibisha Idara ya Usalama wa Rais.
Mwanaume huyo alikuwa amebeba bunduki na kopo la mafuta aliposimamishwa kabla ya kupigwa risasi na maafisa wa Usalama.
Tukio hilo lilitokea jana Jumapili asubuhi, wakati Rais alipokuwa Washington DC. Mshukiwa ametajwa kama Austin T Martin kutoka Cameron, North Carolina.
Familia yake huko North Carolina imeripoti kupotea kwake mapema Jumapili asubuhi, Ofisi ya Polisi eneo la Moore imethibitisha hilo.
Ofisi ya Usalama imesema haina historia yoyote ya uhalifu inayomhusu Martin, lakini alipigwa risasi baada ya kukataa amri.
Chanzo; Itv