Rais Donald Trump wa Marekani amekutana na Rais wa mpito wa Syria Ahmad al-Sharaa na kumsifu kuwa kiongozi "shupavu".
Marekani iliwahi wakati mmoja kumworodhesha Al-Sharaa kuwa "Gaidi Maalum wa Kimataifa" wakimtuhumu kuwa na mafungamano na makundi ya kigaidi.
Trump amekiri kwamba maisha ya zamani ya Sharaa --aliyekuwa akisakwa kwa udi na uvumba na Marekani -- yalikuwa yenye utata, lakini wakati huo huo alimsifia kama "kiongozi shupavu" na akaelezea imani aliyonayo kwake:
Sharaa alikiambia kituo cha televisheni cha Fox News kwamba uhusiano wake na kundi la wanamgambo lilikuwa jambo la zamani na halikujadiliwa kwenye mazungumzo yake na Trump.
Chanzo; Dw