Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

ICE Baada ya Tukio la Mwanamke Kupigwa Risasi

Mwanamke mmoja amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na afisa wa Idara ya Uhamiaji na Forodha ya Marekani (ICE) wakati wa operesheni ya utekelezaji wa sheria jijini Minneapolis, Marekani.

Wizara ya Usalama wa Ndani ya Marekani (DHS) imesema tukio hilo lilitokea wakati mwanamke huyo alipodaiwa kujaribu kuwagonga maafisa kwa gari lake, hali iliyomlazimu afisa wa ICE kufyatua risasi akidai kujilinda.

Hata hivyo, Meya wa jiji la Minneapolis, Jacob Frey, amepinga vikali maelezo hayo ya serikali ya shirikisho baada ya kupitia picha za video za tukio hilo.

Frey amesema tukio hilo lilikuwa la uzembe na lisilo la lazima, akisisitiza kuwa matumizi ya nguvu yalikuwa ya kupita kiasi. Ameitaka ICE kuondoka mara moja katika jiji hilo, akisema uwepo wao unaweka raia katika hatari.

Tukio hilo limezua mjadala mkubwa kuhusu matumizi ya nguvu na mamlaka ya ICE katika miji inayopinga operesheni kali za uhamiaji.

Huku uchunguzi ukiendelea, wanaharakati wa haki za binaadamu na viongozi wa jamii wameitaka serikali ya Marekani kuwawajibisha maafisa waliotumia nguvu kupita kiasi na kulinda usalama wa raia wasiokuwa na hatia.

 

 

Chanzo; Cnn

Kuhusiana na mada hii: