Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Wanawake Kupiga Bila Kuvjwa Sheria Yasainia Taliban

Kiongozi mkuu wa Taliban, Hibatullah Akhundzada, amesaini sheria mpya ya adhabu nchini Afghanistan ambayo inaruhusu wanaume kuwapiga wake na watoto wao, mradi tu vipigo hivyo havisababishi kuvunjika kwa mifupa au majeraha ya wazi mwilini.

Sheria hiyo ambayo imezua taharuki kimataifa, haikuishia hapo, bali imegawanya jamii katika madaraja ya kijamii, ambapo adhabu hutofautiana kulingana na hadhi ya mkosaji.

Kulingana na kituo cha habari cha FirstPost, chini ya mfumo huu mpya, wasomi wa dini hupewa ushauri pekee wanapokosea, watu wa daraja la chini hukabiliwa na vifungo vya gerezani au adhabu za viboko.

Mazingira ya kisheria kwa wanawake yamezidi kuwa magumu, ambapo sasa mwanamke anaweza kufungwa hadi miezi mitatu gerezani ikiwa atatembelea ndugu zake bila ruhusa ya mumewe.

Aidha, mwanamke anapodai kufanyiwa ukatili mahakamani, analazimika kuleta ushahidi akiwa amejifunika mwili mzima na akiwa ameambatana na mlezi wa kiume. 

 

 

Chanzo; Eatv

Kuhusiana na mada hii: