Serikali ya Kenya imeanzisha uchunguzi kufuatia madai kwamba baadhi ya raia wamekuwa wakimiliki au kutumia mabomu ya kutoa machozi—vifaa vinavyopaswa kuwa chini ya udhibiti wa vyombo vya usalama.
Uchunguzi huo umetokea baada ya mikutano kadhaa ya kisiasa kuvurugika, tukio lililoibua maswali kuhusu usalama wa umma na uadilifu wa maafisa wa polisi.
Waziri wa Usalama wa Ndani, Kipchumba Murkomen ameeleza kwamba serikali inachunguza kwa kina jinsi vifaa hivyo vya polisi vinaweza kuwa mikononi mwa raia.
Akizungumza leo mjini Nanyuki, kaunti ya Laikipia, Murkomen amesema vyombo vya usalama vinachunguza uwezekano wa ushirikiano kati ya raia na baadhi ya maafisa wa polisi katika kusambaza mabomu ya machozi.
Chanzo; Dw