Chama kipya kilichoasisiwa na vijana nchini Bangladesh baada ya maandamano makubwa ya mwaka 2024 sasa kinakabiliwa na mgawanyiko mkubwa wa ndani, baada ya kutangaza muungano wa uchaguzi na chama cha Kiislamu.
Chama cha National Citizen Party, NCP, ambacho kilijitokeza kama sauti ya vijana baada ya uasi wa umma mwaka 2024 nchini Bangladesh, sasa kinakabiliwa na uasi wa wazi kutoka ndani.
Zaidi ya viongozi wakuu thelathini wa chama hicho wamepinga hadharani muungano wake wa uchaguzi na chama cha Jamaat-e-Islami, huku baadhi yao wakitangaza kujiuzulu kwa hasira.
Wachambuzi wa siasa wanaonya kuwa hatua hiyo huenda ikaathiri mustakabali wa chama hicho na kuimarisha vyama vya zamani vilivyotawala siasa za nchi hiyo kwa miongo kadhaa.
Chanzo; Dw