Mtalii mmoja kutoka Romania, Ovidiu A., alijikuta matatani mara baada ya kukamatwa na kufungwa gerezani nchini Italia kwa karibu mwezi mzima, baada ya polisi kumchanganya na mhalifu mwingine mwenye jina sawa. Ovidiu, aliwasili katika mji wa Caorle, karibu na Venice, mnamo Agosti 24, akiwa na mkewe na binti zake kwa ajili ya likizo. Lakini mambo yalibadilika ghafla alipokamatwa na polisi wakati akipata chai hotelini.
Kilichomponza ni jina lake ambalo linafanana na mhalifu mwingine kutoka Romania aliyewahi kuhukumiwa nchini Italia kwa kosa la wizi wa kutumia nguvu. Mfumo wa polisi ulitoa tahadhari mara tu jina lake liliposajiliwa hotelini. Baada ya karibu mwezi gerezani, Ovidiu aliachiliwa na kuungana tena na familia yake.
Chanzo; Dw