Siku mbili tangu kuanza muhula mwingine wa masomo nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, shule katika mji wa Uvira, uliotekwa na waasi wa AFC/M23 mnamo Desemba bado hazijafunguliwa. Wazazi walio wengi pia wakihofia usalama wa watoto wao.
Tangu wikendi iliyopita, vijana walioteuliwa na utawala mpya wa AFC/M23 katika eneo hilo wamekuwa wakizunguka vitongoji mbalimbali vya Uvira, wakiwahimiza wazazi kuwarudisha watoto wao shuleni.
Wakati huo huo, shule kadhaa mjini Uvira zinakaliwa na watu waliolazimika kuyahama makazi yao kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya ya Uvira waliokimbia mashambulizi.
Chanzo; Dw