Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

TikTok Yafuta Video Laki Tano za Wakenya

Mtandao wa Kijamii wa TikTok umesema umefuta zaidi ya video laki tano na elfu themanini ( 580,000 ) za Watumiaji wake Nchini Kenya katika kipindi cha kuanzia Julai hadi Septemba 2025, kufuatia ukiukwaji wa miongozo yake ya matumizi (Community Guidelines) katika juhudi za kuimarisha usalama wa Watumiaji na kudhibiti maudhui yasiyofaa kwenye Mtandao huo.

Kwa mujibu wa ripoti ya utekelezaji wa kanuni za maudhui ya robo ya tatu ya mwaka 2025 (Q3 2025 Community Guidelines Enforcement Report), asilimia 99.7 ya video hizo zilitambuliwa na kuondolewa kabla hata hazijapata Watazamaji au kuripotiwa na Watumiaji wengine ambapo asilimia 94.6 ya maudhui hayo yaliondolewa ndani ya saa 24 tangu kuchapishwa.

Mbali na video za kawaida, TikTok pia ilisimamisha mamia ya maelfu ya LIVE za Tiktok ( maudhui ya moja kwa moja) yaliyobainika kukiuka sera zake ambapo Kampuni hiyo imesema kuwa inatumia teknolojia ya akili bandia (AI) pamoja na Timu za ukaguzi wa kibinadamu kufuatilia na kuchuja maudhui yanayochapishwa kila siku.

Baadhi ya sababu zilizopelekea maudhui kufutwa ni pamoja na kuchapisha taarifa za uongo, maudhui ya chuki au uonevu, picha na video zisizo na ridhaa ya Wahusika pamoja na maudhui hatarishi au yasiyofaa kwa umma na akaunti zinazokiuka masharti ya umri au kuhusika na udanganyifu hatua ambayo inaonesha msimamo wa TikTok katika kuhakikisha jukwaa lake linabaki kuwa salama hasa katika soko la Afrika Mashariki ambako matumizi ya mitandao ya kijamii yanaongezeka kwa kasi.

 

 

Chanzo; Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: