Rais wa Colombia Gustavo Petro amesema yuko tayari “kuchukua silaha” iwapo vitisho kutoka kwa Rais wa Marekani Donald Trump vitaendelea, akieleza kuwa amefikia hatua hiyo kwa ajili ya kulinda taifa lake.
Kauli hiyo imekuja baada ya Trump kumtuhumu Petro kuhusishwa na biashara ya dawa za kulevya, madai yaliyoibuka kufuatia operesheni ya Marekani iliyomkamata Rais wa Venezuela Nicolás Maduro.
Petro, aliyewahi kuwa mwanachama wa kundi la waasi la M-19 kabla ya kusalimisha silaha mwaka 1989, amesema aliapa kutobeba silaha tena, lakini anaweza kuvunja kiapo hicho “kwa ajili ya nchi” huku mvutano kati ya Bogotá na Washington ukiendelea kuongezeka.
Chanzo; Cnn