Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mjukuu wa Mandela Adaiwa Kutekwa Gaza

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, ameitaka Israel kuwaachia mara moja wanaharakati wa Afrika Kusini waliokamatwa na jeshi la majini la Israel baada ya kuizuia Global Sumud Flotilla, msafara wa meli uliokuwa ukielekea Gaza kwa ajili ya misaada ya kibinadamu.

Kati ya waliokamatwa ni pamoja na mjukuu wa Nelson Mandela, Nkosi Zwelivelile “Mandla” Mandela, huku taarifa zikithibitisha uwepo wa raia wengine wa Afrika Kusini. Nelson Mandela mwenyewe aliwahi kusisitiza mshikamano na Palestina, akisema "uhuru wa Afrika Kusini hautakuwa kamili hadi Wapalestina nao wapate uhuru wao."

Ramaphosa ameeleza kitendo hicho kama “utekaji” na kulaani hatua ya Israel akisema ni “tukio jingine kubwa la kudhalilisha mshikamano wa kimataifa na Gaza.”
meli moja, Mikeno, iliripotiwa kufanikisha kuvuka na kuingia maji ya Palestina, lakini mawasiliano nayo yamepotea.

 

Chanzo: Global Publishers

Kuhusiana na mada hii: