Rais wa Marekani, Donald Trump, ameitangaza Cuba kuwa kitisho kwa usalama wa taifa la Marekani, na kusaini amri ya rais inayolenga kuimarisha vikwazo dhidi ya taifa hilo.
Kwa mujibu wa amri hiyo, nchi yoyote itakayoiuzia au kuipa Cuba mafuta itaongezewa ushuru na Marekani.
Serikali ya Marekani inaishutumu Cuba kwa kuunga mkono na kusaidia makundi inayoyataja kuwa ya kigaidi, yakiwemo Hamas na Hezbollah, pamoja na kudumisha uhusiano wa karibu na nchi hasimu wa Marekani, zikiwemo Urusi, China na Iran.
Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za utawala wa Trump kuzuia upatikanaji wa mafuta nchini Cuba, bidhaa ambayo ni muhimu kwa uchumi na huduma za msingi za taifa hilo.
Cuba imekuwa ikipata mafuta kutoka kwa wasambazaji wake wakuu, wakiwemo Venezuela na Mexico. Hata hivyo, Mexico ilitangaza mapema wiki hii kuwa imesitisha kwa muda kuiuzia Cuba mafuta.
Chanzo; Crown Media